Latest Posts

SHUGHULI ZA KIUCHUMI HUFIFISHA MALEZI BORA – DKT. MUSA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa, Ali Mussa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo na Taifa kwa jumla kuepuka kujikita kupita kiasi kwenye shughuli za kiuchumi na kusahau jukumu msingi la kulea watoto wao hivyo kuchochea mmomonyoko wa maadili, jambo linalohatarisha kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Dkt. Mussa ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani ambapo Kimkoa yamefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

“Suala la kutafuta kipato ni muhimu, lakini tusisahau kuwa msingi wa taifa lolote ni familia imara. Wazazi wengi wanatumia muda mwingi kwenye biashara na kazi, wakisahau kuwa watoto wao wanahitaji malezi ya karibu,” amesema Dkt. Musa.

Sambamba na hayo, Dkt. Mussa amewataka wazazi kuendelea kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii waliopo katika maeneo yao namna ya kuwasikiliza na kuwasimamia watoto vyema, hasa katika kipindi hiki ambapo teknolojia na mabadiliko ya kijamii yanaathiri mwenendo wa vijana wengi ili kuondoa vitendo viovu ndani ya jamii.

Kwa upande wake, Afisa maendeleo ya jamii  Mkoa wa Morogoro Elizabeth Magagula amesema suala la wazazi kujikita kwenye shghuli za kiuchumi bila kufuatilia malezi ya watoto linasababisha tabia hatarishi kwa watoto na vijana ikiwemo ulawiti, uvutaji bangi, na madawa ya kulevya hivyo Taifa kuzalisha kizazi kisicho bora.

Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu makada CCM TAIFA Bi. Pili Pirahi amewashukuru wadau wote wanaowasaidia watu wenye ulemavu wakiwemo shirika la Lete mabadiliko chanya ulipo (LeMaChU) kwa misaada ya vifaa kwa wahitaji hao.

Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu isemayo: “Mtoto ni malezi:  Msingi wa familia bora kwa Taifa imara” yalilenga kutathmini masuala ya kifamilia ili kutambua matokeo ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika ngazi ya familia na kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!