Latest Posts

SHULE YA SEKONDARI NANDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI

Kukosekana kwa shule ya sekondari ya kata ya Nanda kumetajwa kuwa ni moja ya sababu iliyosababisha wanafunzi kukatisha masomo yao na wengine kutembea umbali mrefu hatua iliyochangia wanafunzi hao kushindwa kufuata ratiba kamili ya masomo na kudhorotesha ukuaji wa elimu.
Kutokana na changamoto hiyo iliyokuwa inawakumba wanafunzi hao kwenye kata hiyo ya Halmashauri ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara serikali imefanya jitihada ya kutatua changamoto hiyo kwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Nanda iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
Baadhi ya wanafunzi hao wameishukuru serikali kwa kuhakikisha inawatatulia changamoto ya kutembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata shule.
Muzwaifa Nafi mwanafunzi wa kidato cha pili amesema hapo mwanzo wanafunzi wakike walikuwa wanapitia changamoto ya kukatisha masomo kutokana na tamaa na vishawishi wanavyokutana navyo njiani kwa kurubuniwa na watu wenye usafiri.
Rashid Rajabu Mkazi wa kata hiyo amesema kabla ya kuwepo kwa shule hiyo ufaulu na idadi ya wanafunzi haikuwa ya kulidhisha kutokana na gharama za nauli ambazo mwanafunzi anatakiwa kutumia kwaajili ya kwenda na kurudi shule ukizingatia na hali ya ngumu ya kimaisha.
Kukosekana kwa shule ya sekondari ya kata kumetajwa kuwa ni moja ya sababu iliyosababisha wanafunzi kukatisha masomo yao na wengine kutembea umbali mrefu hatua iliyochangia wanafunzi hao kushindwa kufuata ratiba kamili ya masomo na kudhorotesha ukuaji wa elimu.
Kutokana na changamoto hiyo iliyokuwa inawakumba wanafunzi hao kwenye kata ya halmashauri ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara serikali imefanya jitihada ya kutatua changamoto hiyo kwa kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari kweenye kata ya Nanda iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
Baadhi ya wanafunzi hao wameishukuru serikali kwa kuhakikisha inawatatulia changamoto ya kutembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata shule.
Muzwaifa Nafi mwanafunzi wa kidato cha pili amesema hapo mwanzo wanafunzi wakike walikuwa wanapitia changamoto ya kukatisha masomo kutokana na tamaa na vishawishi wanavyokutana navyo njiani kwa kurubuniwa na watu wenye usafiri.
Rashid Rajabu Mkazi wa kata hiyo amesema ujenzi wa mradi huo umewaondelea wanafunzi changamoto ya kutembea umbali mrefu na kwenda vijiji jirani kwaajili ya kufata elimu ambapo kabla ya kuwepo kwa shule hiyo ufaulu na idadi ya wanafunzi haikuwa ya kulidhisha kutokana na gharama za nauli ambazo mwanafunzi anatakiwa kutumia kwaajili ya kwenda na kurudi shule ukizingatia na hali ya ngumu ya kimaisha.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Friday Sondasy amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 150, ujenzi ambao umepunguza mlundikano wa wanafunzi katika shule ya sekondari mpotola iliyopo kwenye halmashauri hiyo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Stergomena Tax amewataka wanafunzi na wazazi kutunza mazingira na vifaa vilivyopo shuleni hapo ili vije kusaidia vizazi na vizazi ukizingatia elimu ni ufunguo wa maisha na kuahidi kutoa kompyuta 10.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!