Latest Posts

STEVE NYERERE AVUA GAMBA LA SIASA “SIASA SI KILA MTU”

Msanii maarufu wa filamu na mhamasishaji wa kijamii, Steve Nyerere, ametangaza kujiondoa rasmi kwenye mbio za kisiasa baada ya kushindwa vibaya katika kura za maoni za chama chake, hatua aliyoiita kwa ucheshi wake wa kawaida kuwa “somo la siasa”.

Steve, ambaye jina lake limekuwa maarufu si tu kwenye tasnia ya filamu bali pia kwenye mijadala ya mitandaoni, amesema alipata kura sita pekee kutoka kwa wajumbe wa mkutano wa kura za maoni, idadi iliyomfanya kutafakari upya mustakabali wake kisiasa.

“Baada ya kupata kura sita kutoka kwa wabunge, nimeamua kurudi kazini. Nimewasiliana na bosi wangu Majizzo, nimemwambia nipo tayari kuendelea na kazi rasmi. Siasa si kila mtu kaka,” amesema Steve kwa utulivu ulioambatana na kejeli.

Hatua hiyo imeibua hisia mbalimbali mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wake wamempongeza kwa ujasiri wa kukubali hali halisi, huku wengine wakisema matokeo hayo yanadhihirisha kuwa umaarufu wa kisanii hauwezi kuwa tiketi ya moja kwa moja kwenye mafanikio ya kisiasa.

Kwa muda mrefu, Steve amekuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya kijamii kupitia taasisi yake inayolenga kukuza mawasiliano kati ya wazazi na watoto, na pia kushiriki kampeni mbalimbali za kijamii na burudani.

Wakati sasa akirejea rasmi kwenye shughuli zake za sanaa na harakati, Steve ameacha ujumbe kwa wale wanaotamani siasa kutokana na umaarufu wao:

“Jiandae si kwa fomu tu, bali kwa ukweli wa kisiasa.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!