Latest Posts

SUGU: CCM WANAKOPA SANA TUNAOLIPA DENI LA TAIFA NI SISI WANANCHI

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) ameeleza kukerwa na kitendo cha Serikali ya Tanzania kuendelea kukopa mikopo na kutumiwa vibaya na baadhi ya viongozi badala ya kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.

Ametoa kilio chake hicho wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Isansa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Sugu amesema Taifa limekuwa na viongozi wanaopenda anasa kwa kununua magari ya kifahari kwa ajili ya watumishi wakuu hasa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa na wilaya na Wakurugenzi huku hali ikiendelea kuwa ngumu kwa mwananchi wa kawaida.

Amekosoa safari za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anazokwenda nje ya nchi akiwa na msururu wa watu jambo analosema ni ufujaji fedha za wa-Tanzania.

Pamoja na hayo amewatuhumu baadhi ya viongozi wakiwemo mawaziri kufuja fedha za umma ikiwemo zinazokopwa nje ya nchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!