Latest Posts

TAASISI YA SUPHIAN KUPANDA MITI MILIONI MOJA MKOANI SINGIDA

Shirika la Tanzania Aid Association (TAA) limeendelea na kampeni ya kupanda miti mkoa wa Singida iitwayo ‘Singida Mpya ya Kijani Inawezekana’ ambapo Julai 17, 2024 limepanda miti 600 katika shule za msingi Uwanja wa ndege na Nkungi zilizopo katika Kata ya Ilunda, wilaya ya Mkalama kilomita zaidi ya 100 kutoka Singida Mjini.

Akizungumza na wanafunzi, walimu na viongozi wa serikali waliohudhuria zoezi hilo la upandaji miti, Mkurugenzi Mtendaji wa TAA Suphian Juma Nkuwi amesema mpango wa awamu ya kwanza wa kampeni hiyo ni kupanda miti milioni moja ikiwa ni moja ya mikakati ya taasisi hiyo ya kutunza mazingira dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

“Nyie wanafunzi ndiye baba na mama wa miti hii, itunzeni, tuendelee kumuunga mkono mwanamazingira namba moja Rais Dkt. Samia katika kuirejesha Singida kwenye uoto wake wa asili uliopotea kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya shughuli za kilimo na ufugaji” Ameeleza Suphian.

Naye Diwani wa Kata ya Ilunda kwa jina la Imbele, amemuahidi Suphian kuwa atafuatilia utunzaji wa miti 1000 huku akiwataka wanafunzi kuitunza miti hiyo kwa kuimwagilia maji na kuilinda dhidi ya mifugo na wanyama wengine waharibifu, lakini pia amewaagiza wanafunzi kutoa taarifa wanapowaona wananchi wakiikata miti hiyo.

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa wilaya ya Mkalama Albert Robert na Mhifadhi msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Mkalama ambao wameshiriki kampeni hiyo Abdul Ali na walimu wakuu wa shule za Nkungi na Uwanja wa ndege wameipongeza TAA kwa juhudi zake za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!