Latest Posts

TAHOSSA NA MAAFISA ELIMU RUVUMA WAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII 

Wakuu wa shule za Sekondari Mkoa wa Ruvuma (TAHOSSA) na maafisa elimu wa Wilaya zilizopo Mkoani hapa kwa kushirikiana na wizara ya utalii wametangaza vivutio na vituo kadhaa vya watalii vilivyopo mkoani humo.

Mwenyekiti wa TAHOSSA Mkoani Ruvuma Mwalimu Gerold Ndunguru alisema kuwa Katika kuunga mkono The Royal tour iliyoanzishwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan maafisa elimu na wakuu wa shule wameamua kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mkoani Ruvuma na Nje ya Mkoa wa Ruvuma

Ndunguru alivitaja vivutio ambavyo walivitembelea ni pamoja na Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Safu za Milima Matogoro na Chanzo cha Mto Ruvuma

Na mbuga ya wanyama ya Luhila katika Manispaa ya Songea kisiwa cha Lundo katika Wilaya ya Nyasa, Jiwe la Mbuji katika Wilaya za Mbinga, na vivutio vilivyopo Tunduru na Namtumbo.

Ziara hiyo ilijumuisha zaidi ya wakuu wa shule 130, Maafisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma, Afisa Taaluma wa Mkoa na Afisa Elimu wa Mkoa (REO)

Ndunguru alisema awali aliwashawishi wakuu wote wa shule za sekondari kutoka Mkoa wa Ruvuma kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa kukuza watalii nchini.

Wakuu wa Shule walithamini uwepo wa vivutio kadhaa vya watalii katika mbuga ya Kitaifa ya Mikumi, walishangazwa na uwepo wa miundombinu iliyotunzwa vizuri ndani ya mbuga hiyo kama vile Barabara, uwanja wa ndege na vyumba vya kulala wageni.

Kwa pamoja walimpongeza Rais kwa kutenga fedha mahsusi kwa ajili ya ukarabati na uanzishaji wa miradi ndani ya Hifadhi.

Na kwamba ziara hiyo wameitumia kama njia ya kutoa shukrani kwa Rais kwa kiasi kikubwa cha fedha zilizotengwa kwa shule mbalimbali za Mkoa wetu.

Wakuu hao wa shule wameahidi kutembelea mbuga za wanyama na vituo vingine vya watalii kila wanapopata nafasi katika maisha yao kama ilivyoanzishwa na wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Editha Mpenzile aliwashauri wakuu wa shule kupanga pamoja na wafanyakazi wenzao kutembelea vituo vya watalii kama sehemu ya burudani, kujifunza mambo mbalimbali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!