Latest Posts

TAKUKURU MORO YAWAKUTANISHA PAMOJA WADAU KUKUZA UMOJA KATIKA JAMII

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Morogoro imeandaa futari maalum iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa mkoa huo, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa kiimani miongoni mwa jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakasege amesema kuwa TAKUKURU imekuwa ikiendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa wananchi. Ametaja miongoni mwa misaada hiyo ni kukabidhi mashine mbili za kusaidia watoto njiti, ikiwa ni mwendelezo wa shughuli za taasisi hiyo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Kamati ya Amani mkoa wa Morogoro, Askofu George Pindua, amesema kuwa Waislamu na Wakristo ni kitu kimoja, jambo linalodhihirishwa na ushirikiano wao katika shughuli mbalimbali za kijamii. Alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko wa kidini.

Naye Katibu wa Sheikh wa mkoa wa Morogoro, Nassoro Koba, ameipongeza TAKUKURU kwa kuandaa iftar hiyo, akisema imeonyesha heshima kubwa kwa taasisi hiyo kwa jamii. Pia aliwasilisha salamu za Mkuu wa Mkoa, akishukuru kwa mwaliko huo.

Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Magereza mkoa huo, Peter Laurian Anatory, ameishukuru TAKUKURU kwa kuandaa hafla hiyo ambayo imewakutanisha waumini wa dini mbalimbali. Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa, alisisitiza umuhimu wa Waislamu na Wakristo kuendelea kuiombea Tanzania amani na kudumisha mshikamano uliopo.

Hafla hiyo imeonekana kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha mahusiano na mshikamano miongoni mwa wadau wa mkoa wa Morogoro, hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!