Latest Posts

TAKUKURU YAZINDUA JENGO JIPYA WILAYANI ROMBO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imezindua rasmi jengo lake jipya la ofisi wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, lililogharimu kiasi cha shilingi Milioni 290 ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa katika ngazi ya wilaya.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi wa Rombo, wakiongozwa na  Mgeni rasmi Neema Jamu Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ikulu.

Katika hotuba yake, Mkuu huyo alieleza kuwa jengo hilo ni sehemu ya mkakati wa taasisi hiyo wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

“Jengo hili litasaidia kuongeza ufanisi wa kazi zetu, kuimarisha uwajibikaji, na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa,” alisema Jamu

Aidha, amewataka wananchi wa Rombo kujitokeza kwa wingi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa njia salama, huku wakihimizwa kuwa mabalozi wa uadilifu katika jamii zao.

Kwa upande wake Neema Mwakalyelye,Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kwa kuunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwapatia kiwanja hicho bure ili kuweka ofisini hiyo muhimu katika kutoa elimu na kusaidia kupambana na rushwa kwa ustawi wa wananchi .

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo Raymond Mangwala amewataka wananchi kuachana na dhana potofu ya Mwaka wa uchaguzi kuwa ni mwaka wa mavuno nakujikuta wakiingia katika vitendo vya rushwa

“Kuna wale wananchi wasema kuwa tumalizane,bila gundi karatasi haishiki,tuachane na mambo hayo yanayochochea vitendo vya rushwa hasa kuelekea katika uchaguzi Mkuu mwaka huu” alionya Mangwala.

Jengo hilo la TAKUKURU linatarajiwa kuwa kitovu cha shughuli za uchunguzi, elimu kwa umma, na usimamizi wa masuala yote yahusuyo rushwa katika wilaya hiyo yenye mpaka na nchi jirani ya Kenya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!