Latest Posts

TALGWU WARIDHISHWA KULIPWA KUPITIA HAZINA BADALA YA MAPATO YA NDANI

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeeleza kuridhishwa na hatua ya serikali ya kuwafanya watumishi wa TALGWU kulipwa mishahara yao kupitia hazina badala ya mapato ya ndani kama ilivyokuwa awali, ikieleza kuwa kufanya hivyo ni kurejesha ari ya utumishi kwa taifa lao.

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Mara Dkt. Magreth Shaku amesema katika mkoa wa Mara, watumishi 16 wamebahatika kuingia katika mfumo huo wa malipo ambapo sasa wanaamini watumishi ambao walikuwa hawapati huduma ya bima ya afya watatibiwa, na watakuwa na uhakika wa kupata mafao yao baada ya kustaafu.

“Tunaahidi sasa utumishi bora sisi kwa mkoa wa Mara kutokana na namna Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa msikivu kwa watumishi wake na hili ni jambo ambalo lilikuwa gumu kwa muda mrefu lakini sasa limerejesha furaha zaidi”, ameeleza Dkt. Shaku.

Aidha baadhi ya watumishi wamesema awali hali ilikuwa mbaya kwani walikuwa wakicheleweshewa mishahara na kusababisha kuingia katika mikopo isiyo ya lazima hivyo kuingizwa katika malipo ya mfuko wa serikali itaenda kubadilisha maisha ya watumishi hao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!