Latest Posts

TANESCO MARA: TUITUMIE NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME KUOKOA MAZINGIRA

Katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika katika viwanja vya Mkoa wa Mara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataka watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, wakati wa ziara yake kwenye banda la TANESCO, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Bi. Joyce William, alisema matumizi ya umeme kama nishati safi ya kupikia yana faida kubwa kwa wananchi, hasa watumishi wa umma, kwa kuwa ni rahisi kutumia, salama kwa mazingira, nafuu na inaokoa muda.

Amesema nishati safi ya umeme ni rafiki kwa mazingira, haina moshi, inaokoa muda kwa watumishi na gharama zake ni nafuu ukilinganisha na kuni au mkaa. Tunawahimiza wananchi kuhamasika kutumia umeme kupikia.

 

Huduma kwa Wateja Yaimarishwa: Namba Maalum Bila Malipo

Katika hatua nyingine, Bi. Joyce alitangaza kuwa TANESCO imeanzisha huduma mpya ya simu bure kwa wateja kupitia namba 180, ili kurahisisha mawasiliano na kutatua changamoto kwa wakati.

Amesisitiza kuwa huduma hiyo ni sehemu ya maboresho yanayolenga kuboresha ufanisi wa shirika hilo, kuongeza uwazi na kuhakikisha wateja wote wanahudumiwa kwa wakati.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!