Latest Posts

TANESCO RUVUMA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UMEME ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA BORA

Na Stephano Mango, Songea.
Shirika la umeme Nchini Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limejidhatiti katika maboresho ya huduma wanazozitoa kwa kuwekeza katika utoaji huduma kidigital lengo ni kuendana na mabadiliko ya  teknolojia pamoja na kuwekeza katika nguzo za zege ambazo ni imara zitakazodumu kwa muda mrefu.
Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja, Afisa uhusiano na huduma kwa wateja wa Tanesco Mkoani Ruvuma Alan Njiro, amesema katika maadhimisho haya wamejikita kuleta mabadiliko ya huduma zao kutokana na teknolojia jinsi ilivyorahisisha kutoa huduma zao kidijiti.
Njiro amesema kuwa jambo hilo linamuwezesha mteja kufanya maombi ya umeme  awapo nyumbani bila kumlazimu kufika ofisini na hivyo kuwarahisishia wateja waliopo Vijijini ambao walikuwa wanatumia muda mrefu na gharama kubwa kufuata huduma za Shirika hilo
Amesema kwa sasa umeme upo wa uhakika ukilinganisha na miaka iliyopita hivyo kwani wanauwezo wa kuwahudumia wateja wengi kutokana na uwepo wa vyanzo vikubwa vya umeme ikiwemo Bwawa la Mwl. Julius Nyerere ambalo kwa kiasi kikubwa litaondoa adha ya umeme.
Amewashukuru wateja wao kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho walikuwa wanakabiliwa na umeme wa mgao huku matarajio yao nikuboresha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.
Akizungumzia kuhusiana na ukomo wa maboresho ya mfumo wa luku, amesema yanatarajia kufikia ukomo tarehe 30 mwezi Novemba hivyo ni muhimu kwa wateja wote kuhakikisha wanafanya maboresho hayo ambayo yanalengo lakuendana na viwango vya luku vya kimataifa ili kuendelea kufurahia huduma zao.
Diwani wa Kata ya Lilambo Yobo Mapunda amewapongeza sana Tanesco kwa jitihada yao kuu katika kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana hadi vijijini.
Mapunda amewaomba Tanesco waendeleze kusambaza huduma ya umeme hasa kwenye maeneo ya miradi mikubwa ya ujenzi inayoendelea sehemu mbalimbali na katika maeneo ambayo viwanja vingi vinatolewa kwa wananchi ili kuwezesha maendeleo.
Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja nchini yanafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba chini ya Kauli mbiu isemayo ni zaidi ya matarajio, ambapo hii, yametanguliwa na mkutano wa ndani wa shirika hilo pamoja na utoaji baadhi ya zawadi kwa wateja wanao ingia na kutoka ndani ya ofisi hiyo katika juma zima la maadhimisho hayo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!