Latest Posts

TANESCO SACCOS YAKABIDHI MASHUKA 500 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA

Chama cha Akiba na Mikopo cha TANESCO (TANESCO SACCOS) kimesema kitaendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, hususan katika sekta ya afya.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi mashuka, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO SACCOS, Bw. Omary Ramadhan, amesema chama hicho kimekabidhi mashuka 500 yenye thamani ya takribani Shilingi milioni 23 kwa hospitali mbalimbali, kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.

Amesema TANESCO SACCOS imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kupitia miradi ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile inachokipata kupitia wanachama wake.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TANESCO SACCOS, Bw. Hilary Andrea, ameeleza kuwa misaada kama hiyo itaendelea kutolewa katika maeneo mengine nchini kulingana na mahitaji yaliyopo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ameipongeza TANESCO SACCOS kwa mchango huo, akibainisha kuwa utasaidia kuboresha huduma za afya na kugusa maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!