Latest Posts

TANZANIA YAJIVUNIA UWEPO WA KIWANDA CHA KWANZA CHA MABOMBA YA SINDANO (SYRINGE)

Na; mwandishi wetu

Katika kile kinachodhihirisha kuimarika kwa sekta ya uwekezaji nchini, katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru wa nchi ya Tanzania, kwa mara ya kwanza Tanzania inashuhudia kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa mabomba ya sindano (Syringe) cha ndani

Kiwanda hicho cha ‘Medical Dawlia Limited’ kilichopo Kisarawe II, wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam, Jumatano Desemba 11.2024 kimetembelewa na Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri aliyeambatana na Mkurugenzi mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) Mavere Tukai ambapo kwa pamoja wamefanya ukaguzi na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo ikiwemo kushuhudia mchakato wa uzalishaji wa mabomba hayo

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema uwepo wa kiwanda hicho ni matokeo ya wazi kabisa ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo kwa kiasi kikubwa imeweka mazingira rafiki ya kuchangamkiwa naa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi

Amesema baada ya kuingia madarakani mwezi Machi 2021 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara kwenye mataifa mbalimbali nchini ikiwemo Misri na Uturuki ambapo kutembelea kwake kwenye nchi hizo ndiko kulikopelekea kushawishi wawekezaji wa kiwanda hicho kuja nchini na sasa matunda yake yameanza kuonekana

Aidha, Teri ametoa wito kwa wawekezaji wengine kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini zinazochochewa na utashi wa Rais Dkt. Samia wa kuimarisha sekta hiyo

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) Mavere Tukai amesema uwepo wa kiwanda hicho ni fursa kubwa kwa MSD kwa kuwa wao ndio wateja wakubwa wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba nchini na kwamba mara zote wamekuwa wakilazimika kuagiza mabomba ya sindano (syringe) kwa asilimia 100 kutoka nje ya nchi jambo ambalo kwa sasa litakuwa tofauti

Amesema kwa kuanza MSD imetoa oda ya kupatiwa mabomba ya dawa (Syringe) yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania ambapo wanatarajia kupokea mzigo huo juma lijalo

Sambamba na hilo, amesema kutokana na mahitaji yao oda hiyo ni ya awali tu, hivyo wameingia makubaliano miongoni mwa taasisi hizo mbili (MSD na Kiwanda cha Medical Dawlia Limited) ambayo yatapelekea MSD kuwa mtaja mkuu wa bidhaa inayozalishwa kiwandani hapo kwa kuagiza mabomba ya aina tofauti ikiwemo 2 mil, 5 mil na 10 mil

Naye, Ibrahim Adel Khalile ambaye ni mmoja wa wamiliki na waanzilishi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa ubia kati ya raia wa mataifa mawili tofauti ya Misri na Uturuki amesema kwa pamoja walianza mchakato wa ujenzi mnamo mwaka 2022 lakini uzalishaji wake umeanza takribani mwaka mmoja uliopita, na kwamba kwa kiasi kikubwa wanafurahishwa na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini

Khalile amemshukuru Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri na taasisi anayoiongoza kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanawasaidia wawekezaji hao kufikia malengo waliyokusudia, ambapo anasema TIC imekuwa ikichukua hatua kwa haraka pale inapohitajika ikiwemo kushughulikia changamoto zinazojitokeza

Pia, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kimsingi ndiye kiranja mkuu katika kuongoza na kufanikisha sekta ya uwekezaji Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!