Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila ameagiza TARURA Morogoro kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa daraja la Lukuyu lililopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro ifikapo Agosti 2024 ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo kusafirisha mazao ikiwamo ndizi na kubeba mbogamboga kichwani.Mativila ameyasema hayo Juni 19, 2024 wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa wananchi kuondokana na changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.
Daraja la Lukuyu limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 70 linaenda kuwa mwarobaini kwa wakazi wa kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro.