Latest Posts

TCRA YAANIKA ONYO KALI WATETEZI TV KWA KUCHAPISHA HABARI ZA ‘KICHOCHEZI’ NGORONGORO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeionya Watetezi TV kwa kurusha habari zinazodaiwa kuwa za kichochezi kupitia chaneli yake ya YouTube, ikisema kuwa licha ya kituo hicho kuandikiwa barua ya onyo tarehe 5 Aprili 2024, kimeendelea kukiuka Sheria, Kanuni, na Masharti ya Leseni kwa kurusha tena maudhui yanayokinzana na sheria tarehe 30 Julai 2024.

Katika barua ambayo Jambo TV tumeishuhudia, ikiandikwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaomiliki kituo hicho, TCRA imetaja kauli za Watetezi TV kama ile ya “Serikali imetunyanganya uhuru wa kupiga kura Ngorongoro, yani ni afadhali hata wafungwa” – Olemangi, kuwa ya kichochezi.

Katiba barua hiyo iliyoandikwa Agosti 23, 2024 TCRA imesema kuwa tarehe 12 Agosti 2024, Watetezi TV ilirudia kosa lingine kwa kuchapisha maudhui ya namna hiyo kupitia chaneli yake ya YouTube, yenye maelezo “NEC mnavunja Sheria za Uchaguzi” Vijana Ngorongoro watoa msimamo huu, wasisitiza NEC haijatenda haki”.

Maudhui hayo yameelezwa kuwa ya upande mmoja wa habari, yakiacha kutoa fursa kwa upande wa serikali au mamlaka husika kutoa maelezo yao kuhusu shutuma zilizotolewa na mwananchi aliyekosoa hali hiyo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Utangazaji Mtandaoni 2020, kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022, TCRA imesema kuwa Watetezi TV imekiuka Kanuni za 9 (a) na 12 (a) (i).

TCRA imeagiza kituo hicho kuondoa mara moja maudhui hayo kutoka chaneli yake na kutoa maelezo ya kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuendelea kukiuka sheria huku ikikipa siku saba (7) kutoa maelezo tangu wakati taarifa hiyo ilipotolewa.

TCRA imesema kuwa endapo Watetezi TV itapuuza au kukaidi kutekeleza maelezo hayo, mamlaka hiyo haitasita kuchukua hatua zaidi za kisheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!