Latest Posts

TEF YAELEZA KUSIKITISHWA NA KUKIFO CHA ALI MOHAMMED KIBAO

 

 

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kusikitishwa na taarifa za kifo cha Kada wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) na Mjumbe wa Sekretarieti, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amewapa pole familia ya ndugu Kibao, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wana – CHADEMA wote kwa kuondokewa na kiongozi wao katika mazingira ya kusikitisha, pia Watanzania wengine waliofikwa na madhila ya namna hiyo.

Kwenye taarifa hiyo, Balile amemuomba Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aunde Tume ya Majaji kuchunguza wimbi la utekaji na mauaji nchini.

“Tunamwomba Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aunde Tume ya Majaji kuchunguza wimbi la utekaji na mauaji, ambalo lilianza kwa mtu mmoja mmoja sehemu mbalimbali nchini, likahamia kwawatotona sasa watu wanashushwa kwenye magari ya abiria na kuuawa,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia Balile ameshauri uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kujitafakari i iwapo unastahili kuendelea kuwapo wakati tuhuma hizi nzito za watu kutekwa zikiendeleakusikika sehemu mbalimbali nchini.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!