Latest Posts

TEF YAWAPONGEZA KABUDI, MAKONDA NA MWINJUMA KUTEULIWA KUONGOZA WIZARA YA HABARI

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa pongezi kwa viongozi wapya wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akiwamo Profesa Palamagamba Kabudi aliyeteuliwa kuwa Waziri, pamoja na Mhe. Paul Makonda na Mhe. Hamis Mwinjuma walioteuliwa kuwa Manaibu Mawaziri wa wizara hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Novemba 18, 2025 na Mwenyekiti wa jukwaa hilo Deodatus Balile, amesema uteuzi huo unaonesha imani ya Serikali katika kuwapa nafasi viongozi wenye uzoefu, ubunifu na weledi katika masuala ya utawala na mawasiliano ya umma.

Vilevile jukwaa hilo limesema linaamini uongozi huo mpya utaimarisha utekelezaji wa majukumu ndani ya wizara, hususan katika kuendeleza sekta ya habari na tasnia za ubunifu.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema Wizara ya Habari ina nafasi muhimu kama kiunganishi kati ya Serikali na wananchi, hivyo uteuzi huo unatarajiwa kuleta msukumo mpya katika maboresho ya mifumo ya upashanaji habari na maendeleo ya tasnia.

Ameendelea kwa kusema kuwa, TEF iko tayari kutoa ushirikiano wa karibu wa kitaalamu ili kuhakikisha malengo ya Serikali katika kuifanya sekta ya habari kuwa chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanatekelezwa kwa ufanisi.

“TEF inawatakia utekelezaji mwema wa majukumu yenu mapya. Mungu ibariki Tanzania,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!