Latest Posts

MALIMA AITAKA JAMII KUTETEA HAKI ZA WATOTO WA KIKE

Katika juhudi za kuhakikisha mtoto wa kike na mwanamke wanapata heshima na nafasi wanayostahili katika jamii, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amesisitiza umuhimu wa kulinda makundi haya na kuhakikisha wanapewa haki zao za msingi, hususan watoto wa kike wanaonyimwa fursa ya kupata elimu.

Akizungumza Novemba 5, 2025, na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Morogoro, Malima alisema kuwa jamii haiwezi kuwa imara na yenye maendeleo bila kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki yake ya elimu na kuondolewa kwenye mnyororo wa ukatili, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike ili kujenga jamii yenye heshima, usawa na utu.

Pia amesema kuwa hali ya amani na utulivu mkoani humo imeimarishwa kikamilifu, ikianzia siku ya upigaji kura unaoendelea, ambapo wananchi wanaendelea na maisha yao ya kawaida, pamoja na kupata elimu ya kutunza amani na kuepuka kuiga vitendo visivyofaa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Mchungaji Norbert Mbuya, amesema kanisa hilo limeanzisha nyumba maalum za kuwahudumia watoto wa kike na wanawake waliokumbwa na ukatili, ambapo tangu kuanzishwa kwa mradi huo, watoto 89 tayari wamepewa huduma na hifadhi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!