Latest Posts

TFS TARIME KUGAWA MICHE YA MITI LAKI MOJA BURE

 

Wakala wa huduma za misitu Tanzania katika wilaya ya Tarime mkoani Mara unatarajia kugawa miche zaidi ya laki moja bure inayoendana na mazingira ya wananchi ikiwa ni mkakati wake wakuhakikisha inalinda uoto wa asili wilayani humo.

 

Kauli hiyo imetolewa na Bw.Charles Masawe katika kikao cha wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Tarime mkoani Mara ambapo amesema zoezi la utoaji bure wa miche hiyo limekuwa niendelevu kwa wananchi wa maeneo husika.

 

“ Tupo hapa kwaajili ya kikoa cha kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na tunaendelea kutoa elimu kuwasisititiza kwaajili ya umuhimu wa kutunza mazingira na mikakati kwa wilaya yetu yumekuwa tukigawa micheze na kwa mwaka fedha ulioisha tuligawa miche elfu sabini na Nne”Charles Masawe Mhifadhi misitu Tarime.

 

Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amesisitiza upandaji wa miti nakutunzwa katika maeneo ya wananchi binafsi pamoja na maeneo yaliyotengwa huku akitaka kukomeshwa uchomaji wa moto ovyo katika misitu pamoja na uvunaji holela wa miti.

 

 

“Niwaombe TFS na wasimamizi wote wananchi wetu wanahitaji kupata elimu katika eneo hili naniwaombe msiwaonee wananchi katika jamboi hili badala yake muongeze nguvu kwenye elimu zaidi”Alisema Meja Edward Gowele Mkuu wa wilaya ya Tarime.

 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza elimu inayotolewa na wakala wa misitu huku wakiomba serikali kuendelea kutoa elimu ambayo itaondoa migongano baina ya wananchi na wahifadhi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!