Latest Posts

TFS WINO WATWAA UBINGWA BONANZA LA MICHEZO

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Shamba la Miti Wino wamemaliza Bonanza la Michezo la TFS, lililowakutanisha timu nane kutoka kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, kwa lengo la kuelimisha wananchi kuhusu uhifadhi wa misitu, madhara ya moto na kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji.

Katika mchezo wa fainali, TFS Wino walitwaa ubingwa baada ya kuifunga Magingo FC kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90.

Akizungumza wakati wa hitimisho la bonanza Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama, amesema mashindano hayo ni zaidi ya burudani kwa kuwa yanatumika kutoa elimu muhimu ya uhifadhi.

Amesema misitu ni muhimili wa uchumi wa kijani, akawataka wananchi kuachana na matumizi ya moto kwenye maandalizi ya mashamba hususan msimu huu wa kilimo, kwani husababisha uharibifu wa rasilimali na mazingira.

Kwa upande wake, Mhifadhi Muandamizi wa Shamba la Miti Wino, Glory Kasmir, alisema bonanza hilo ni njia shirikishi ya kuwaunganisha wananchi na TFS kupitia elimu ya ulinzi wa misitu, mbinu salama za maandalizi ya mashamba na udhibiti wa moto misituni, sambamba na kuinua vipaji vya michezo kwa vijana.

Baadhi ya wakazi na washiriki wa mashindano hayo walisema elimu waliyoipata itawasaidia kuimarika kiuchumi kupitia kilimo salama na shughuli rafiki kwa mazingira, huku wakiahidi kuwa mabalozi wa uhifadhi katika vijiji vyao kwa kutekeleza mafunzo ya TFS katika maisha ya kila siku.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!