Latest Posts

TIC YAENDELEA KUVUTIA UWEKEZAJI KUTOKA CHINA

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendelea kuvutia uwekezaji kutoka nchini China, kikiwa na lengo la kuvutia kiasi cha Dola za Marekani bilioni 3 sawa na Shilingi trilioni 7 kwa mwaka kutoka taifa hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri ameeleza hayo wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni inatoa huduma za Kisheria ya Yingke (China) ambayo ina wanasheria zaidi ya 55,000 ikitoa huduma kwa wateja zaidi ya 1,500,000.

Teri amesema kuwa kuanzia mwaka 2013 mpaka 2023 TIC imepata uwekezaji zaidi ya Dola za Marekani zaidi ya bilioni 10 sawa Shilingi trilioni 27 kutoka China, TIC ikipata Dola bilioni moja, Shilingi trilioni 3 kila mwaka

Teri ameeleza kuwa TIC itaendelea kuvutia uwekezaji kutoka China kwenye sekta mbalimbali lakini kipekee lengo likiwa kuvutia uwekezaji kwenye sekta za madini na utalii.

Kwa upande wake, Mwenyekikiti wa Bodi Kampuni ya Yingke Law Firm, Xiangrong Mei amesema kupitia mashirikiano hayo na TIC, wataendelea kuleta wawekezaji tofauti nchini Tanzania ili kuinua uwekezaji.

Kongamano hilo limekutanisha wawekezaji na kampuni zaidi 20 na wenzao wa nchi ya Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!