Latest Posts

TIC YATWAA TUZO YA TAASISI BORA INAYOCHANGIA MAENDELEO YA BIASHARA NCHINI

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea Tuzo ya Taasisi Bora inayochangia maendeleo ya Biashara nchini yaani Best Trade facilitor kwa lugha ya Kiingereza.

Tuzo hiyo iliyotolewa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) usiku wa tarehe 23 Julai 2024 imepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Gilead Teri.

Sambamba na kupokea tuzo hiyo, Teri ameshiriki katika mjadala maalumu wa kujadili hatua muhimu na mambo yanayohitajika kufanywa ili kuboresha ustawi wa nchi.

“Ni heshima kubwa kwa mchango huu kwa kuwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya biashara nchini” Amesema Teri.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!