Serikali ya Wilaya ya Wilaya ya Nyasa imeitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuchukua hatua za haraka kuvuna mamba katika Ziwa Nyasa kufuatia kuongezeka kwa matukio ya wananchi kushambuliwa na kuuawa na wanyama hao wakati wakifanya shughuli zao za kila siku ziwani.
Wakiongea katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma baadhi ya viongozi na wazee wa mila katika wilaya ya Nyasa wamesema matukio ya watu kuuwawa na mamba katika ziwa Nyasa ni mengi hali inayohatarisha utalii katika ziwa hilo hivyo wamewataka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuwavuna mamba katika ziwa hilo pia ushauri umetolewa kuwashirikisha wazee wa mila katika zoezi hilo.

Erick Mongi Kamanda wa TAWA mkoa wa Ruvuma amesema tayari wameanza mpango wa kujenga vizimba viwili katika ziwa Nyasa ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto ya watu kuuwawa na mamba katika ziwa Nyasa.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amesema licha ya TAWA kujenga vizimba katika ziwa Nyasa lakini upo umuhimu wa kuwashirikisha wazee wa mila katika kutatua changamoto ya mamba katika ziwa hilo.
