Latest Posts

TUMBILI NA NYANI WAMEKUWA KERO, BIASHARA YA KUUZA VIUMBE HAI KUREJEA

Changamoto ya uwepo wa wanyama waharibifu wa mazao imeendelea kuripotiwa katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba akiwa Mkoani Kilimanjaro ambapo wakazi wa Wilaya ya Rombo wameomba wanyama aina ya nyani na tumbili kupunguzwa au kuuzwa.

Akijibu changamoto hiyo iliyoripotiwa na wananchi Februari 19, 2026, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kipindi Cha nyuma Serikali ilikuwa na biashara ya viumbr hai wa porini na ilitokea changamoto mwaka 2016 jambo hilo likasitishwa na kupokea maelekezo ya serikali kwa kufanyia kazi suala hilo.

“Changamoto hii inayojitokeza inatulazimu kuwaua tumbili au nyani wetu na tumeshauwa zaidi ya 247 sasa kuliko kuwaua bure serikali kupitia Mhe.Rais Samia ametuelekeza sisi Wizara ya Maliasili na utalii tufanyie kazi changamoto iliyotokea ili kurejesha biashara ya kuuza viumbe hai ili nyani au tumbili hawa badala ya kuwaua tuweze kuwauza ili kuingiza mapato kuondoa changamoto iliyosemwa na Wananchi wetu”, amesema Dkt.Kijaji.

Amesema kuwa wakati wanashughulikia jambo hilo Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA wanaendelea kulifanyia kazi ili kutengeneza vikundi mbalimbali vya kijamii vya ulinzi ili kuzuia nyani hao kuingia katika makazi na mashamba ya wananchi.

Awali akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Mkazi wa Masekini Kata ya Marangu Kitowo ameeleza kuwa changamoto kubwa inayo wakabili wakulima ni uwepo wa nyani na tumbili wanaoharibu mbegu na mazao hali inayopelekea hasara

“Tunaomba tupate usaidizi wa kuondoa hawa wanyama waharibifu waliosambaa katika maeneo yetu kwani wanafukua mbegu na kula au kukwanyua mazao machanga”alisema

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!