Latest Posts

“TUMIENI VYUO VIKUU KUFANYA TAFITI ZA KILIMO“ PINDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda ameitaka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro kuhakikisha wanatumia vyuo vikuu hasa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa ajili ya tafiti za kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuweza kuleta tija kwa Taifa

Pinda ameyazungumza hayo Agosti 8, 2024 mkoani Morogoro katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane mkoani humo ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa wa kutumia tafiti ili kuweza kuleta manufaa kwa wakulima nchini.

“Mikoa hii ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro ambayo imeunganisha kanda ya Mashariki ni wakati sasa wa kutumia tunu hizi mlizopewa hasa vyuo vikuu kama SUA kwa ajili ya tafiti ili kuweza kuleta tija kwa Taifa”, ameeleza Pinda.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema kuwa mpango wa mkoa huo ni kufikiria kilimo cha miaka 20 ijayo hasa katika kudhibiti mazingira ili kupata maji ya kutosha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!