Latest Posts

UCHUNGUZI MAUAJI YA KIBAO: MNYIKA AOMBA KUAHIRISHA WITO WA POLISI KWA SABABU YA KIKAO CHA CHADEMA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameomba kuahirishwa kwa wito wa polisi uliomtaka kufika katika ofisi za Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Mkoa wa Kinondoni, tarehe 18 Septemba 2024.
 
Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na wakili wake, Hekima Mwasipu wa Matwiga Law Chambers kwa Ofisi hiyo ya upelelezi, Mnyika hangeweza kuhudhuria wito huo kutokana na kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kinachofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 17 na 18 Septemba 2024.
 
“Mteja wangu anakiri kupokea barua yako ya tarehe 16 Septemba, 2024 iliyofikishwa kwake tarehe 17 Septemba, 2024 asubuhi, yenye Kumb. BE.210/1032/01/271 yenye kichwa cha habari hapo juu, ikimtaka kufika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoa wa Kipolisi Kinondoni tarehe 18 Septemba, 2024 saa nne asubuhi”, inasomeka sehemu ya barua hiyo, iliyopokelewa na ofisi za polisi tarehe 18 Septemba 2024.
 
Barua hiyo iliandikwa baada ya kupokea wito wa kufika polisi kuhusu jalada la mauaji ya kada wa CHADEMA Ally Mohamed Kibao, kesi ambayo inazidi kuvutia hisia kali kutoka kwa wananchi wa Tanzania na jamii ya kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!