Latest Posts

UFALME WA ESWATINI WAWASILI NCHINI KUJIFUNZA UENDESHWAJI PSSSF

Ufalme wa Eswatini pamoja na Waziri wa Utumishi umewasili nchini ukiambatana na wabunge na watendaji wa sekta ya hifadhi ya jamii ili kujifunza namna Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma (PSSSF) unavyoendeshwa .

Akizungumza Ijumaa Julai 19, 2024 Jijini Dodoma mara baada ya kupokea ujumbe  wa watu tisa kutoka Ufalme wa Uswatini , Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru amesema lengo ni kubadilishana uzoefu wa uendeshaji mfuko kati ya nchi hizo mbili.

“Eswatini wapo na sisi hapa Dodoma kujifunza mambo makubwa ikiwemo kufahamu namna ambavyo sisi PSSSF tumeweza kufanya mageuzi makubwa tangu kuanzishwa kwa mfuko, tumezungumza nao kuhusu mageuzi katika huduma tunazotoa kwa wanachama. Sasa huduma zinapatikana katika mfumo wa kidigitali mwanachama anaweza kujisajili alipo na namna ambavyo tumeweza kutengeneza mikakati mahsusi ya kushughulika na changamoto ambazo tulikutana nazo siku za nyuma.” Amesema Badru.

Aidha, amesema wameelezwa namna ya kusimamia shughuli za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba kunapowekezwa mitaji ya mifuko lazima ielekezwe maeneo yenye tija yanayoweza kuzalisha na uwekezaji uwe na mchango katika maendeleo na uchumi wa nchi.

“Hayo ndio baadhi ya mambo ambayo tumezungumza nayo wayasingatie wakati wakitekeleza mikakati yao ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii na kuboresha mfuko wao katika falme za Eswatini, tutaendelea kuwapa usaidizi wa kitaalam wakati wanatekeleza mikakati hiyo, wametuchagua sisi tufanye hivyo.” Amesema Badru.

Kwa upande wake, Waziri wa Utumishi wa Eswatini, Mabulala Maseko amesema wamekuja nchini kupata uzoefu wa namna ambavyo PSSSF imekuwa inapambana kuhakikisha mfuko wake unaendelea kuwa imara na unatoa huduma bora kwa wanachama.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!