Latest Posts

KUSEMA ALI KIBA ‘MBANA PUA’ KULIVYOMUWEKA MASTER J JUU YA KAA LA MOTO

Joachim Kimario maarufu kama Master J ni miongoni mwa watanzania walioweja mchango mkubwa katika tasnia ya burudani Tanzania kuanzia muziki wa Taratibu, Bongo Flava, Kwaya, na bendi.

Master J amefanya kazi kubwa ya kushiriki kuibua vipaji vya wasanii kupitia jukwaa la Bongo Star Search. Wiki moja iliyopita (26/02/2025) palikuwa na tamasha kubwa la tuzo liitwalo Trace Music Award lililofanyika Zanzibar.

Trace Award ni jukwaa kubwa la tuzo barani Afrika hivyo kufanyika Tanzania ilikuwa ni heshima kubwa na nafasi ya wasanii wetu kuonyesha vipawa vyao. Jambo la tofauti kwenye tamasha hili wasanii hawaendi tu kuburudisha kwa nyimbo zao kupigwa kama inavyokuwa kwenye show zao za kawaida, Ila wanapaswa kuimba nyimbo zao live.

Msanii wa kwanza wa Tanzania kupanda jukwaani alikuwa ni Marioo akiimba wimbo wake wa Unanchekesha kisha ukafuata wimbo wa Nairobi aliomshirikisha msanii wa Kenya Bienaimesol.

Baada ya hii performance maoni yalikuwa hasi sana kwenye mitandao kuwa Bien alienda kumuokoa Marioo wengine wakisema hakufanya mazoezi na wengine wakidai sauti ya studio na live ni mbingu na ardhi. Baadae walitumbuiza Harmonize, Diamond Platnumz na Zuchu. Lakini show zao hazikutumika kama mfano kama ilivyo kwa Marioo.

Kwanza tumpongeze Marioo kwa kuweza kuaminiwa na jukwaa kubwa kama hili na kuweza kufanya alichofanya, pili tukubali Bienaimesol na Fally Ipupa walifanya show nzuri kwa kuimba vyema zaidi tatu wasanii wetu wakubali kufanya kazi ya ziada kwenda kufanya mazoezi ya live performance watuheshimishe.

Tuachane na tuzo sasa baada ya tuzo zilisambazwa video clips mtandaoni zikimuonyesha Legend Master J alipowahi kusema Bien akija Tanzania atavuruga sana wasanii wetu na ni kweli alifanya hivyo huku baadhi ya watu wakimuomba msamaha kwenye comment kwa sababu kipindi anasema hilo suala alitolewa kauli chafu sana.

Wakati wa nyuma kwenye mahojiano aliyowahi kufanya Master J aliwahi kusema Diamond Platnumz ni mburudishaji mzuri lakini muimbaji ni Ali Kiba (Diamon is good entertainer but Ali Kiba is a good musician)

Februari 28 ilikuwa kilele cha Bongo star search pengine hii siku Master J ataikumbuka sana. Kabla ya tamasha kuanza alifanya mahojiano na kituo cha Simulizi na Sauti (SnS) na kwenye mahojiano hayo alitamka kuwa muimbaji wa live ni Barnaba na wasanii wengine wa THT lakini Ali Kiba ni “mbana pua”.

Kauli ya Ali Kiba ni mbana pua ilimuibua Kiba kupitia instagram yake ns kuandika maneno makali dhidi ya master J akifikia kumuita majina ambayo pengine watu hawakutarajia “Umekuwa ukiropoka sana mitandaoni bila kujiheshimu wala kuheshimu watu sijui unajiona nani yani kama vile wewe ndio unapandisha watu daraja katika maisha mabadiliko yako ya akili unayaweka hadharani unataka tujiskie vipi sisi tunao kuheshimu unaropoka sana siku hizi umesahau brand yako uliyoitengeneza miaka mingi unahitaji kunyamaza sio kila kitu watu wasubiri utasema nini”

Maoni ya watu yapo yaliyomuunga mkono Ali Kiba na wapo waliomtaka kulinda brand yake kwa kuacha management yake ichukue hatua. Lakini utakubaliana na mimi kwamba Ali Kiba huwa hajibu mambo yanayomhusu mtandaoni na ni mara chache sana yeye kufanya hivyo.

Machi 03 Master J alifanya mahojiano na chombo cha habari cha Crown FM ambacho Kiba ni Rasi wa Media hiyo na kwenye mahojiano aliyofanya na Mwijaku MJ alikiri kuwa siku anasema Kiba ni mbana pua alikua amelewa hivyo akaomba radhi.

Hivi ndivyo Mic zinaweza kukupandisha daraja na kushusha thamani yako mapema sana.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!