Latest Posts

UJERUMANI YASHIKWA KIGUGUMIZI KUMUUNGA MKONO VON DER LEYEN URAIS HALMASHAURI EU

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekwepa kutamka kuwa atamuunga mkono Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen katika ombi lake la kuwania muhula mwingine wa kiti hicho.

Taarifa iliyochapishwa kupitia mtandao wa shirika la habari la kimataifa la Ujerumani (DW) mapema Jumanne Juni 11, 2024 imeeleza kuwa hayo hayo yametokea siku moja tu, baada ya uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) ambapo Scholz amerudia msimamo wake wa awali kwamba nafasi ya Rais wa Kamisheni lazima uwe na uungwaji mkono wa msingi wa wingi wa kidemokrasia wa kijadi katika Bunge la Ulaya.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Berlin nchini Ujerumani akiwa na Rais wa Chile aliyetembelea nchini humo Gabriel Boric, Scholz amesema hata hivyo upo uwezekano wa kuzingatia kumuunga mkono sambamba na wagombea mbalimbali wa nafasi za juu za Umoja wa Ulaya (EU) katika siku za usoni.

Von der Leyen, mwanasiasa wa Ujerumani ambaye pia ni Waziri wa zamani kutoka chama cha kihafidhina cha Conservative Christian Democrats (CDU), ametoa wito kwa vyama vya kidemokrasia na vya kiliberali vya Umoja wa Ulaya (EU) kuunga mkono azma yake ya kuwania tena kiti cha Halmashauri Kuu ya umoja huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!