Latest Posts

UKOSEFU WA TAKWIMU NI SAWA NA KWENDA VITANI BILA SILAHA

 

Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imesisitiza matumizi ya Takwimu kwani ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Julai 23,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanaasha Khamisi Juma wakati wa ziara ya mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kamati hiyo pamoja na Watendaji Kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.

 

“Takwimu sahihi ni muhimu kwa Maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kuendelea kuzitumia Kwa maslahi mapana ya Taifa,” Amesema

 

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amesema ni maono ya Rais Dkt. Samia na Dkt.Huseein Ally Mwinyi kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza takwimu rasmi nchini.

 

“Sensa ya watu na makazi ya iliyofanyika mwaka 2022 imeleta heshima kwasababu ilifanyika kisasa na kwa ufasaha wa Hali ya juu kutokana na maona ya viongozi wetu ,”

Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juma Makungu Juma amesema takwimu ni muhimu kwa Maendeleo ya nchi.

Amesema ukosefu wa takwimu ni sawa na kwenda vitani bila siraha lazima utashindwa ndio maana viongozi wakuu wanasisitiza matumizi ya takwimu.

“Tunapoenda kuelimisha umuhimu watakwimu itasaidia kutoa elimu kwa wananchi. Kumekuwa na ushurikiano mzuri kati ya Ofisi ya takwimu ya Tanzania bara na Zanzibar Kwa maslahi ya Taifa,”Amesema.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!