Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma umempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mohammed Monni kwa kutekeleza na kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo Ikiwemo Kufungua shule 13 mpya za Msingi, shule 7 mpya za sekondari, Zahanati 11, pamoja na vituo vya afya.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo Mhandisi Jalali Mkunji wakati wa kikao cha mwisho wa mwaka cha Bazara hilo kilichofanyika Wilayani hapo.
Mhandisi Mkunji amesema Mbunge Monni amefanya kazi kubwa pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa kwa CCM pamoja na kuisaidia jumuiya kutimiza wajibu wake.
Amesema jitahidi hizi zimefanikiwa kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi na kuzielekeza maeneo yote ya nchi.