Latest Posts

UVCCM MARA KUWALINDA NA KUWASEMEA WATEULE WA CCM WA URAIS

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara Mary Daniel amesema watahakikisha wanawalinda kwa nguvu zote na kuwasemea vyema viongozi walioteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa kugombea katika nafasi za Urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Zanzibar kutokana na maendeleo makubwa waliyoyaahidi kuyatekeleza kwa kiasi kikubwa.

Kauli hiyo imetolewa na na mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa wa mara Marry Daniel Wakati akitoa tamko la kuunga mkono uamuzi uliofanywa na mkutano mkuu maalum wa CCM wa kumteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mbali na Rais Samia, mkutano huo pia ulimteua Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza kwa nafasi hiyo huku Dkt. Hussein Mwinyi akiteuliwa kuwa mgombea nafasi ya urais kwa upande wa Zanzibar.

Akitoa tamko hilo mjini Musoma Jumapili Januari 26,2025 Musoma, Mwenyekiti wa umoja huo, Mary Daniel amesema kwa kauli moja wanawapongeza viongozi hao kwa kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi hizo na kwamba wapo tayari kuwalinda na kuwaombea kura.

“Kazi ndio inaanza, sisi umoja wa vijana wa mkoa wa Mara mbali na kuwapongeza wagombea wetu na kitoa tamko la kuunga mmono uamuzi wa mkutano mkuu maalum sasa tunalo jukumu moja tu mbele yetu ya kutafuta kura ili kuwawezesha wagombea wetu wanashinde kwa kishindo katika uchaguzi ujao,” amesema

Amesema vijana hao wana uhakika wa chama chao kupata ushindi kutokana na namna ambavyo serikali imeweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia kubwa.

“Kwa miaka mitatu mkoa wetu umepokea zaidi ya Sh1.22 trilioni ambazo zimetolewa na serikali kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kijamii na sote ni mashuhuda wa miradi hiyo hivyo hatuna shaka tunapojiandaa kuanza kupita kwa wananchi kwaajili ya kuomba kura,” amesema.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara,Patrick Chandi amesema baada ya maamuzi ya mkutano huo kazi ya wana CCM sasa ni kutafuta kura kwaajili ya chama hicho kuendelea kushika dola.

“Hatuna cha kumlipa mama zaidi ya kumpa kura kwasababu ametufanyia mambo mengi,ilani imetekelezwa vizuri sana, hapa kwetu tumeshuhudia mambo mengi mazuri yaliyofanywa hivyo kwa pamoja tunawajibika kumuumga mkono na si vinginevyo,” amesema

Chandi ametolea mfano ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari ambapo awali kila mwaka wazazi walikuwa wakilazimika kuchanga fedha kwaajili ya ujenzi wa madarsa lakini hivi sasa suala hilo linatekelezwa na serikali

Katibu wa Kamati ya Maridhiano na Amani ya mkoa wa Mara, Juma Masirori amesema wanaunga mkono tamko hilo la UVCCM Mkoa wa Mara na kwamba suala hilo linalenga kuimarisha amani na utulivu wa nchi.

“Mama Samia amefanya mengi mazuri kwaajili ya nchi yetu,kubwa zaidi ni suala la amani kwani utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo unaoendelea mbali na kulenga kutoa huduma bora kwa wananchi lakini pia unalenga kuboresha amani kwani penye maendeleo pana amani” amesema

Amesema amani ya nchi ni bora kuliko kitu kingine hivyo wao kama viongozi wa dini jukumu lao kuu ni kuona amani inalindwa ili wananchi waweze kuoata fursa ya kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!