Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) limetoa onyo kali kwa baadhi ya wanasiasa na asasi zinazowatumia vibaya vijana kwa maslahi yao binafsi. Katika taarifa iliyotolewa baada ya kikao cha baraza hilo jijini Dodoma, UVCCM walisema kuwa hawatavumilia matendo hayo.
“UVCCM hatutavumilia vitendo vya kuwatumia vijana kwa kuharibu mshikamano wa taifa letu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Baraza hilo pia liliwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi unaokuja. “Kujitokeza kupiga kura ni wajibu wa kila kijana, na UVCCM tutahakikisha tunawaunga mkono,” walisema.

UVCCM pia walitoa pongezi kwa serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa jinsi zinavyowatumikia wananchi kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.