Latest Posts

UWANJA WA NDEGE MUSOMA KUKAMILIKA SEPTEMBA, SERIKALI YALIPA BIL. 5.2 KWA KAYA 58 KUPISHA UJENZI

Ujenzi na ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Musoma unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 35 unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba mwaka huu, huku serikali ikiidhinisha malipo ya shilingi bilioni 5.2 kwa kaya 58 kupisha eneo la ujenzi wa jengo la abiria.

Akitoa taarifa hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, aliyefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara, Vedastus Maribe, amesema kuwa tayari asilimia 80 ya gharama za mradi huo zimeshalipwa na serikali, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga nchini.

Kanali Mtambi ameagiza mkandarasi kuhakikisha uwanja huo unakamilika kabla ya Septemba, akisema kasi ya utekelezaji inaonesha inawezekana kukamilika kwa wakati huo.

“Mradi huu ni wa kimkakati na unaleta fursa kubwa kwa Mkoa wa Mara — kutokana na shughuli za madini, hifadhi na utalii. Hatutaki kuchelewa hata siku moja,” amesema Kanali Mtambi.

Amesisitiza kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutarahisisha huduma za usafirishaji kwa abiria na mizigo, kuongeza fursa za kiuchumi, na kuvutia wawekezaji kutokana na hadhi ya kipekee ya Mkoa wa Mara kibiashara, kiutalii na kiuwekezaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!