Jumuiya ya wa Wanawake Tanzania (UWT), umelaani vikali vitendo vya ukatili na unyanyasaji anavyodaiwa kufanyiwa binti mkazi wa wilayani Temeke, Dar es Salaam.
Inadaiwa binti hiyo, mkazi wa Kata ya Makangarawe, wilayani Temeke, Dar es Salaam, alibakwa na kulawitiwa na vijana watano, kisha video ya vitendo hivyo kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda alitoa tamko la kulaani vitendo hivyo jana baada ya Agosti 5, mwaka huu, kusambaa video tatu tofauti zikionesha msichana akifanyiwa vitendo vya kikatili na udhalilishaji mkubwa.
“Kamwe, hauwezi kuvifumbia macho vitendo vya unyanyasaj, ukatli na udhalilishaji kama huo, kwa sababu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vinaleta athari zinazodumu kwa muda mrefu kwa waathirika,” alisema.
Chatanda aliongeza kuwa: “Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) inalaani vikali vitendo vya ukatili na unyanyasaji vilivyorekodiwa kupitia picha mjongeo (video clip) na kusambazwa katika mitandao ya kijamii. Kamwe! hatuwezi kuvifumbia macho vitendo vya unyanyasaji, ukatili na udhalilishaji kama huu kwasababu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vinaleta athari zinazodumu kwa muda mrefu kwa waathirika.” alisema.
Alisema tukio hilo la kikatili linatweza heshima ya mwanamke na kuchafua taswira ya nchi.
Mwenyekiti huyo alisisitiza uchunguzi wa kina na uwajibikaji wa haraka kutoka katika mamlaka zinazohusika kuhakikisha haki inatendeka na watuhumiwa wanafikishwa katika vyombo vya sheria.
Pia, alisema msaada wa kisaikolojia unapaswa kutolewa haraka iwezekanavyo kwa mwathirika wa tukio hilo.