Latest Posts

VIGOGO CHADEMA ‘WABURUZWA’ MAHAKAMANI KWA KUKIUKA AMRI YA MAHAKAMA KUU, WAMO HECHE NA MNYIKA

Na; mwandishi wetu

Katika hali isiyotarajiwa aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohammed na wenzake wawili (Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu) wamefungua maombi madogo kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche na wenzake wanane wakidai kwamba wahusika (watuhumiwa) wamekiuka maelekezo ya Mahakama hiyo yaliyotolewa dhidi yao Juni 10 mwaka huu

Maombi hayo madogo yaliyopewa namba 8960 ya mwaka 2025 yanatokana na kesi ya msingi namba 8323 ya mwaka 2025 inayoendelea Mahakamani hapo chini ya Jaji Hamidu Mwanga

Kupitia maombi hayo yaliyofunguliwa Oktoba 02.2025, walalamikaji kupitia Wakili wao Mulamuzi Patrick Byabusha wamedai kuwa walalamikiwa wameendelea kuitisha na kuandaa mkutano mbalimbali ya ndani, kutoa maelekezo ya kazi za kisiasa yanayohusiana na hicho, na kuzungumza na vyombo vya habari jambo ambalo ni kinyume na marufuku iliyotolewa na Mahakama hiyo

Itakumbukwa kuwa, kufutia uwepo wa kesi ya msingi namba 8323/2025 inayoendelea Mahakamani hapo iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA, Juni 10 mwaka huu Mahakama ilipiga marufuku wadaiwa kujihusisha na shughuli zozote za kisiasa na kiutendaji, kutumia raslimali za chama na mambo mengine yote yanayoshabihiana na hayo, hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi

Utolewaji wa amri hiyo ambao ulikuwa sehemu ya maombi ya wadai yaliyowasilishwa Mahakamani hapo, pia iliwagusa wasaidizi wa wadaiwa, mawakala wao na wote wanaofanya shughuli zao kwa namna moja au nyingine chini ya mwavuli wa CHADEMA

Ikimbukwe kuwa, katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa chama hicho kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa mali, raslimali fedha nk, sambamba na hilo inadaiwa kuwa chama hicho kimekuwa kikitoa kauli zinazoashirikia udini, ukosefu wa usawa wa kijinsia na viashiria vya kuvuruga muungano jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya CHADEMA, Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

Sambamba na Heche, walalamikiwa wengine kwenye maombi hayo madogo ni John Mnyika (Katibu Mkuu), Rose Mayemba (Mjumbe wa Kamati Kuu), Brenda Rupia (Mkurugenzi wa Habari na Uenezi), Hilda Newton (Mjumbe wa Baraza Kuu), Twaha Mwaipaya (Mwenezi wa zamani wa BAVICHA), na Gervas Benard Lyenda (Afisa kutoka Kurugenzi ya Habari na Uenezi), wengine ni Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA

 

Inaelezwa kuwa, endapo Mahakama itawakuta na hatia walalamikiwa ya kukiuka amri yake, huenda wahusika wakapelekwa gerezani hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!