Latest Posts

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA AJIRA MRADI WA MAJI MLUNDUZI, DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene amewataka vijana wa Kata ya Mlunduzi hususani Kijiji cha Chinyanghku kuchangamkia fursa ya ajira katika mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya Shilingi milioni 900 hadi kukamilika kwake unaoendelea kijijini hapo.

Simbachawene ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mlunduzi kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika Vijiji vya Chinyika, Chaludewa na Chinyanghuku Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

“Ninawaomba vijana mbadilike nendeni mkafanye kazi katika mradi wa maji, ifike hatua wakazi wa maeneo haya muanze kutafuta hela kwa bidii badala ya kubaki watazamaji ilhali vijana wa maeneo mengine wakichangamkia fursa hiyo” amesisitiza Simbachawene.

Amesema ni aibu kumuona kijana akibeti na kulewa pombe za kienyeji kuanzia asubuhi hadi jioni ilihali kuna fursa ya kuweza kujiongezea kipato amewata wakafanye kazi katika mradi.

Aidha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa heshima aliyowapa wananchi wa Kibakwe kwa kuwaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Amesema chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumekuwa na utitiri wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Jimbo hilo huku akitaja kata za Milimani ambako ni maeneo magumu kufikika lakini kwa sasa huduma za kijamii zimeendelea kusogezwa kwa kasi.

“Maeneo ya Milimani ikiwamo Kata ya Lufu, Mangaliza na Galigali mwaka 2005 kulikuwa gizani, kulikuwa hakuna barabara punda pekee ndio walitumika kama njia pekee ya usafiri ila kwa sasa kuna barabara za uhakika magari makubwa na madogo yanakwenda bila shida yoyote na sasa zile sehemu korofi TARURA wapo mzigoni wanatengeneza barabara ya zege ” Amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema Rais Samia anataka aione Kibakwe yenye nuru kiuchumi na mabadiliko.

“Uwepo wa Taasisi za Umma katika maeneo hayo magumu ya Milimani ikiwemo ujenzi wa Shule za Sekondari unaoendelea Man’galiza Lufu na Galigali kutachagiza maendeleo huku akiwataka wananchi kukaa kimkakati ili wawe wanufaika namba moja wa fursa hizo” Ameeleza Simbachawene.

Akizungumzia hatua hizo za maendeleo katika Jimbo zima la Kibakwe Mhe.Simbachawene amesema Kibakwe ya sasa imefunguka kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi huku huduma za kimsingi zikiwa zinapatikana mahali popote bila kujali jiografia ya eneo husika.

Amesema ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) pamoja na ujenzi wa Vituo vya afya ni ushahidi tosha wa jinsi Rais Samia Suluhu Hassan alivyojitoa kwa wananchi wa Jimbo la Kibakwe.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!