Latest Posts

VIONGOZI CHADEMA TABORA WATOA MSIMAMO DHIDI YA G55: “NI WASALITI WA MSIMAMO WA CHAMA”

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Tabora na Kanda ya Magharibi, wakiwemo watia nia wa ubunge katika majimbo mbalimbali, wamejitokeza hadharani kulaani vikali kundi la G-55 lililoibuka ndani ya chama hicho, wakilituhumu kukiuka misimamo halali na maazimio yaliyopitishwa katika mikutano ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili, Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Sikonge, Felix Lyata, amesema kundi hilo linachukuliwa kama wasaliti kwa kuwa wanapingana na msimamo wa chama kuhusu kampeni ya No Reforms, No Elections.

“Sisi tutaendelea kuwatambua hawa G55 kama ni wasaliti kwa mujibu wa Katiba ya Chama na mwelekeo wetu. Kama Tabora na Kanda ya Magharibi, msimamo wetu ni mmoja – No Reforms, No Elections. Hatuna mpango wa kumvumilia yeyote anayepinga hadharani msimamo huu,” amesema Lyata kwa msisitizo.

Kwa upande wake, Peter Kilomba, mtia nia wa ubunge kupitia CHADEMA, ameeleza kuwa kundi hilo linakwenda kinyume na muongozo wa chama, na akasisitiza wao wanaunga mkono kwa dhati misimamo ya chama hususan katika kutetea maslahi ya wananchi na demokrasia ya kweli.

Naye Mbunge wa Wananchi Mpanda Vijijini, Emmanuel Lusomba, ameongeza kuwa bado hawana imani na baadhi ya viongozi wa chama katika Kanda ya Magharibi, akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora kuwa ni miongoni mwa wanaoshukiwa kuwa sehemu ya kundi la G55 lenye lengo la kudhoofisha msimamo wa chama. Hata hivyo akizungumza mapema na Jambo TV, Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Tabora, James Kabepele, alikanusha kuhusika na waraka wa vuguvugu la G55 linalodaiwa kupinga kampeni ya No Reforms No Election, akisisitiza kuwa hakuwahi kuweka saini kwenye waraka huo wala kuonesha nia ya kugombea jimbo lolote.

Pamoja na msimamo huo, viongozi hao wamebainisha kuwa maandalizi ya ujio wa viongozi wa juu wa CHADEMA katika Kanda ya Magharibi yamekamilika kwa kiasi kikubwa, na wamewataka wanachama kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye ziara hiyo muhimu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!