Latest Posts

VIONGOZI WA BODI ZA VYAMA VYA USHIRIKA KILIMANJARO WATAKIWA KUTAMBUA WAJIBU WAO KATIKA VYAMA

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kilimanjaro Jacqueline Senzighe amewataka viongozi wa bodi za vyama vya yshirika wa mbogamboga kutambua wajibu wao katika vyama na kutowaachia watendaji kuendesha vyama hivyo.

Ameeleza kuwa chama ni cha wanachama na si cha watendaji hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanakisimamia chama chao katika shughuli zote za utendaji.

“Ili kiwe chama bora ni lazima viongozi wazingatie maadili ya uongozi kwani kiongozi ndiye muonesha njia na kiongozi ndiye anaweza kujenga au kubomoa chama chake ikiwa hatokuwa na maadili” -Jacqueline.

Ameeleza hayo tarehe 10/06/2024 wakati akifungua mafunzo yaliyoratibiwa na tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania (TCDC) ya wajumbe wa vyama vya ushirika vya mbogamboga yaliyofanyika mkoani humo.

Aidha, Mrajis msaidizi huyo amewataka viongozi hao kuzingatia sheria zote za uendeshaji wa vyama watakazofundishwa ambazo ndio miongozo ya uendeshaji wa vyama.

“Tume haijawaacha wakiwa, hivyo msiwe na hofu ya mtaendeshaje vyama vyenu, niwatoe wasiwasi, TCDC imetoa miongozo ambayo itawaongoza na ni vyema ikafuatwa ili mjenge hivyo vyama viwe imara” -Jacqueline

Naye, Mrajis msaidizi (Uhamasishaji) Ibrahim Kadudu ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hivyo ili kuelewa kiundani dhana za ushirika na kujua vyama vya mbogamboga vinaendeshwaje.

Mafunzo hayo yamehusisha taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Kilimo, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCu), Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!