Latest Posts

VYAMA VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KURAHISISHA UTENDAJI KAZI

Vyama vya ushirika vimetakiwa kuendana na usasa kutokana na mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia duniani hivyo matumizi ya TEHAMA yatarahisisha utendaji kazi katika vyama hivyo ili kuwa na maendeleo yenye tija.

Hayo yamebainishwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro Cesilia Filimin wakati akifungua Jukwaa la maendeleo ya ushirika Mkoani Morogoro ambapo amesema kuwa vyama hivyo vinatakiwa kuhama katika mifumo ya analojia hususan matumizi ya karatasi katika kutunza takwimu na kazi zingine badala ya kutumia mifumo ya kidijitali ili kurahisisha utendaji na utunzaji wa taarifa muhimu za wanachama wa vyama hivyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoani Morogoro Iddi Bilali amesema jukwaa hilo limekuwa likifanyika kila mwaka huku likiwa na mafanikio makubwa katika kubadilishana uwezo pamoja na kujadili changamoto na mafanikio katika utendaji ili kuendelea kuongeza ufanisi katika utendaji na uendeshaji wa vyama hivyo.

Kwa niaba ya wanachama wa vyama vya ushirika Florentina Kachelwa amesema kabla ya kuingia katika vyama vya ushirika wakulima walikubwa na changamoto za pembejeo za kilimo, mbolea na mbegu bora ambazo zimetatuliwa kwa kiasi baada ya kuingia katika vyama vya ushirika huku akiiomba serikali kuendelea kuongeza nguvu katika utatuzi wa changamoto hizo ili kuwawezesha wakulima wanaotegemea vyama hivyo kuendesha maisha yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!