Latest Posts

WAANDIKISHAJI WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI NA MIONGOZO KATIKA CHAGUZI

Waandikishaji wa orodha ya wapigakura ngazi ya Vitongoji wametakiwa kila mmoja kwa nafasi yake awajibike kwenye eneo lake ipasavyo kwa kuzingatia maelekezo na miongoni waliyopatiwa ili waweze kufanikisha zoezi hilo.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Uchaguzi Shabanho Mwaipopo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyasa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Waandikishaji wa Orodha ya wapiga kura ngazi ya Vitongoji, watakaotekeleza zoezi la uandikishaji wapiga kura linalotarajia  kuanza  tarehe 11 hadi  20 Oktoba 2024.
Amesema kwamba wamekutana hapo ili kupeana miongozo mbalimbali itakayo wawezesha kusimamia kwa uadilifu uandikishaji.
“Nawataka washiriki, kuzingatia Sheria, Kanuni , miongozo na maelekezo ya Serikali katika zoezi hilo ili kufikia lengo la kuandikisha watu wote wenye sifa za kupiga kura” alisema Mwaipopo.
Aidha,  amewataka  kusikiliza kwa makini wakati wawezeshaji wakiwasilisha mada mbalimbali kuhusu zoezi la uandikishaji ili waweze kufahamu sifa na  utaratibu wa kuwaandikisha wapiga kura.
Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Nyasa amesema kuwa hategemei kusikia mtu ameharibu kazi kwa uzembe wake na badala yake kazi ikamilike vizuri kwa mujibu wa sheria za nchi
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika makao makuu ya Tarafa katika Tarafa  tatu za  Ruhekei, Mpepo na Ruhuhu na washiriki kutoka Kata 20 za Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wamehudhuria lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza Majukumu yao.
Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ndio dira ya Uchaguzi Mkuu wa hapo mwakani, hivyo kinachotakiwa ni kusimamia vizuri taratibu zote za Uchaguzi kwa kuzingatia 4R za mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!