Latest Posts

WADAU WA ELIMU WATAKA KITENGO CHA ELIMU YA WATU WAZIMA KITENGEWE BAJETI YA KUTOSHA

News, Njombe.

Serikali imetakiwa kuongeza bajeti kwa ajili ya kitengo cha elimu ya watu wazima ili kuboresha na kuongeza ufanisi kwenye kitengo hicho ambacho kimekuwa na msaada mkubwa katika kuongeza uelewa kwa wanafunzi waliocheleweshwa kujiunga na masomo kwa njia ya mfumo rasmi.

Wito huo umetolewa na Yusuph Yahaya ambaye ni afisa taaluma sekondari wilaya ya Wanging’ombe wakati wa maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima wilaya ya Wanging’ombe yaliyofanyika katika kata ya Ilembula wilayani humo.

“Ili mpango wa elimu ya watu wazima uweze kuboreshwa zaidi,kitengo kinashughulika na programu nyingi hivyo tunaomba kwa mwaka wa fedha 2024 – 2025 kitengo kitengewe bajeti ya kutosha na walimu wanaofundisha madarasa ya memkwa wapewe mafunzo ya mara kwa mara ili kuhusisha taarifa zao”amesema Yahaya.

Kwa upande wake Damasi Kavindi afisa tarafa ya Wanging’ombe,kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo amewataka wananchi kuhamasisha maendeleo ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi na kumuagiza mkurugenzi kuhakikisha anatenga bajeti za ndani kwa ajili ya kitengo hicho.

“Mkurugenzi hakikisheni mnatenga bajeti katika bajeti zenu kwa ajili ya mipango mbalimbali ya elimu ya watu wazima ili kuhakikisha kitengo kinafanya kazi bila kuyumba”amesema Kavindi

Mariano Mhule na Nuru Mkenja ni baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya msingi Igelehedza wanaishukuru serikali kwa mpango huo wa kutoa elimu kutokana msaada mkubwa wanaopata ili kuongeza maarifa bila ubaguzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!