Latest Posts

WADAU WA SAMAKI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUWEKEZA ZAIDI KWENYE VIZIMBA

 

Wadau wa samaki jijini Mwanza wameiomba Serikali kuwekeza fedha zaidi katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kutatua changamoto ya upungufu wa samaki sokoni.

 

Wakizungumza na Jambo Tv wakiwa kwenye eneo la ufungaji wa samaki kwa njia ya vizimba lililopo Luchelele jijini Mwanza mbali na kueleza namna wanavyonufaika na ufugaji huo baadhi ya wachakataji wa samaki pia wamedai kuna haja ya Serikali na wadau mbalimbali kuwekeza katika ufugaji huo ili kukidhi mahitaji ya walaji.

Akiunga mkono hoja hiyo huku wakiendelea na zoezi la uvunaji wa samaki kwenye vizimba vyao vinne Mwenyekiti Bodi ya Chama cha Ushirika Nyanza, Leonard Lyabalima amesema pamoja na Serikali kuwekeza kwenye vizimba lakini bado mahitaji ya samaki ni makubwa kutokana na idadi ya watu kuzidi kuongezeka.

 

Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mwanza, Hilda Boniphace ameelekeza viongozi wa Chama cha Ushirika Nyanza kuwekeza zaidi kwenye ufugaji huo ili kuunga mkono jitihada za Serikali na kutatua changamoto ya upungufu wa samaki sokoni.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!