Latest Posts

WADAU WAELEZA UMUHIMU WA ELIMU YA NISHATI SAFI, WAITAKA SERIKALI KUWEKEZA NGUVU HUKO

Wadau wa sekta ya nishati safi na salama ya kupikia wamesema kuwa moja ya sababu za Watanzania kuendelea kutumia nishati za kupika ambazo si rafiki wa mazingira ni uelewa mdogo juu ya umuhimu wa nishati safi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro katika kikao kilichowakutanisha wadau wa nishati safi na salama ya kupikia kupitia mradi wa Inclusive Green Economy (IGE) msimamizi wa mradi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Aloyce Hepelwa ametoa ushauri kwa Serikali kuendelea kutoa elimu ya kusisitiza matumizi ya nishati safi kwa wananchi.

“Watumiaji wa nishati chafu hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya nishati safi hivyo ni wakati sasa wa Serikali kuweka nguvu katika utoaji elimu juu ya nishati safi ili kuweza kunusuru mazingira “, amesema Hepelwa.

Nao baadhi ya wakazi wa mkoa Morogoro wameiomba serikali kupunguza gharama ya nishati safi za kupikia ili kumuwezesha kila mwananchi kutumia nishati hizo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!