Latest Posts

WAFANYABIASHARA WA KOROSHO WAOMBWA KUTOSIKILIZA MANENO YA WATU WENYE NIA MBAYA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoa wa Mtwara imeombwa kuongeza vifaa ili kuongeza ufanisi zaidi kwenye shughuli za usafirishaji wa korosho.

Akizungumza Disemba 10, 2024 kwenye ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za usafirishaji wa korosho ghafi zinazofanywa na bandari hiyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara Saidi Nyengedi amesema kutokana na uzalishaji wa zao la korosho kuwa mkubwa ipo haja ya mamlaka hiyo kuongeza vifaa ili utendaji kazi wao ukawa madhubuti zaidi.

Hata hivyo Nyengedi amekanusha taarifa za baadhi ya watu wanaodai kuwa makasha ya kusafirishia korosho hayatoshi bandarini hapo na kusema kuwa makasha matupu yaliyopo ni mengi na bado bandari inatarajia kupokea meli yenye makasha elfu 1500 ndani ya wiki hii.

“Watu walikuwa wanalalamika kwamba usafirishaji unakwenda taratibu na makasha hayatoshi, lakini nimejionea mwenyewe kasi inayokwenda, inayofanyika, makasha yaliyopo matupu ni mengi mno na wiki hii kuna meli inaleta makasha elfu 1500. Kuna meli nyingine zitaendelea kuleta makasha, kwahiyo upungufu wa makasha haupo na kazi zinafanyika kwa ufanisi.”Amesema Nyengedi.

Aidha amewaomba wafanyabishara wa korosho kuendelea kutumia bandari hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya watu wenye nia mbaya na bandari hiyo kwani vifaa vipo vya kutosha na viongozi wake wamejipanga kwa ajili ya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Pia amewataka wakulima wa zao hilo kuendelea kuzalisha korosho kwa kuzingatia ubora ili biashara hiyo iendelee kunufaisha, kuleta tija na maendeleo kwa wananchi wote.

Ferdinand Nyathi Meneja wa Bandari ya Mtwara amesema hadi sasa wamefanikiwa kusafirisha korosho ghafi zaidi ya tani 12,500, na hadi kufikia Disemba 20, 2024 wanatarajia kusafirisha korosho ghafi tani laki 200,00.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!