Latest Posts

WAGANGA WA TIBA ASILI WALAANI UKATILI UNAOFANYWA KWA WATU WENYE UALBINO

Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (UWAWATA) umelaani vikali vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye ualbino ikiwamo kujeruhiwa, kuuawa na kupotezwa kusikojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi Juni 6, 2024 jijini Dodoma na Lucas Mlipu, Katibu Mkuu wa umoja huo inasema miongoni mwa sababu zinazochangia ongezeko la matukio hayo ni imani potofu zinazohusisha ushirikina.

“UWAWATA tunalaani vitendo hivi vya kikatili na vyenye kukiuka katiba ya nchi yetu pamoja na sheria za nchi yetu ambavyo havikubaliki kabisa kuendelea katika jamii zetu , hivyo basi rai yangu ni kuhakikisha wale wote wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili wanaviacha mara moja” Amesema Mlipu.

Aidha umoja huo umetoa onyo kwa matapeli wanaotumia mwamvuli wa tiba asili na wanaojihusisha na matukio hayo ya kitapeli kupitia upigaji wa ramli chonganishi kuacha mara moja huku ukisisitiza kuwa watu wenye ualbino wana haki ya kuishi kama wengine.

Hivi karibuni kumezuka matukio kadhaa ya watu wenye ualbino kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwamo tukio la mtoto wa miaka miwili Asimwe Novat wa kijiji cha Bulamula, Kitongoji cha Mbale, Kata na Tarafa ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!