Latest Posts

WAGOMBEA WAOMBWA KUFANYA KAMPENI ZENYE MAADILI NA KUNADI SERA ZA MAENDELEO

Baadhi ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara wamewaomba wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za Vijiji/Vitongoji kufanya kampeni zenye maadili na sera zitakazo leta maendeleo kwenye jamii husika.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti ili kufahamu namna ambavyo wakazi wa halmashauri wamejiandaa na kampeni pamoja na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Ally Mbaraka mkazi wa halmashauri hiyo amesema kipindi hiki cha kampeni anatarajia kusikiliza sera bora zenye usawa na ushawishi zisizohitaji vurugu matusi na uchonganishi kutoka kwa wagombea wa vyama mbalimbali.

Saidi Mponda mkazi wa Mihambwe amesema “wanapokuja kutuomba tuwateuwe wakiwa na maneno yenye changamoto ya maendeleo katika wilaya yetu na nchi yetu hao ndio tutawasikiliza, hatutarajii kuona wagombea wanao kuja na sera kutuingiza kwenye tatizo mabaya hilo hatutegemei lakini pia zile sera zitekelezeke, tutawapa mamlaka ya kuwapitisha ahadi zitekezwe.”Amesema Mponda

Naye Agnes Komba mkazi wa mtaa wa Matogoro amesema  amejiandaa kusikiliza sera za wagombea wote kutoka kila chama ili aweze kumpata kiongozi ambae atampigia kura na kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi ili kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Tandahimba Ibrahim Rashid, amewasihi wanachama wote kufuata kanuni na taratibu za vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu,zenye haki,upendo na amani kwa ajili ya mustakabali wa maisha ya wanatandahimba.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Tandahimba Karim Mbita ametoa msisitizo kwa wagombea wote kufanya kampeni na kistaarabu na kupongeza uongozi wa wilaya kwa kuweka mifumo rafiki ya usalama kwa ajili ya wagombea kufanya kampeni kwa usalama zaidi

Naye Muigizaji Maarufu Nchini Makwaya (maarufu Bambo) ametumia sanaa yake kuhamasisha wakazi wa Tandahimba ili kujitokeza kwenye kampeni wasikilize sera zitakazonadiwa na wagombea wa nafasi mbalimbli za uongozi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!