Latest Posts

WAHITIMU JKT RUVU WAAHIDI KULINDA RASIMALI ZA TAIFA NA KUJENGA UCHUMI

Vijana wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Oparesheni Miaka 60 ya Muungano kikosi namba 832 KJ Ruvu, wameahidi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kujenga uchumi wa nchi.

Wahitimu hao wamesema mafunzo ya jeshi waliyopata kwa kipindi cha wiki 12 yamewawezesha kujifunza maadili ya utii, uzalendo, na uadilifu.

Hilda Edward akitoa risala kwa niaba ya wahitimu, amesema kuwa wamepata stadi za maisha na mafunzo muhimu kuhusu umuhimu wa kulinda rasilimali za taifa.

“Tunaahidi kumsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga uchumi imara kwa manufaa ya taifa letu,” amesema Hilda.

Wahitimu hao walionesha shukrani zao kwa wakufunzi wao, kwa kuwapatia ujuzi na maarifa ya kilimo, ufugaji, na michezo. Vilevile, walikula kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia na kuahidi kudumisha uzalendo na nidhamu waliyofundishwa.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, aliwataka wahitimu kwenda kutumia fursa walizopata kupitia mafunzo hayo na kuendeleza uzalendo na uaminifu kwa taifa. Kunenge alieleza kuwa mafunzo ya JKT ni msingi wa kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa taifa na kusimamia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Solitina Bernad Nshushi, aliwapongeza vijana hao kwa kukubali kushiriki mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria, akisema kuwa wamejijengea msingi imara wa uzalendo na uwajibikaji kwa taifa.

Kamanda wa Kikosi cha Ruvu JKT, Kanali Peter Elias Mnyani alibainisha kuwa wahitimu hao wamejifunza stadi mbalimbali za maisha na wamekidhi vigezo vya kuwa watumishi wa taifa popote watakapopelekwa. Aliongeza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia katika kuimarisha usalama na maendeleo ya nchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!