Latest Posts

WAJASIRIAMALI GEITA WAJENGEWA UWEZO WA KURASIMISHA BIASHARA

Na Joel Maduka, Geita.

Imeelezwa kuwa kuna madhara makubwa yanayoweza kumpata mfanyabiashara endapo hatachukua hatua ya kurasimisha biashara yake, ikiwemo biashara kushindwa kukua pamoja na kukosa fursa ya kupata mikopo itakayomsaidia kukuza uchumi wake.

Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Huduma za Kodi, Fedha na Biashara kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya FINACTAX Associate mkoani Geita, Hamis Kashilila, wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wananchi wa Manispaa ya Geita juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara.

“Mfanyabiashara ambaye hajarasimisha biashara yake anakuwa amejifungia milango mingi ya maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha, kuaminika kwa wateja, pamoja na fursa za kibiashara zinazotolewa na serikali au wadau wengine wa maendeleo,” amesema Kashilila.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wenye Viwanda (TCCIA) Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi, amesema kuwa ni vyema kwa wafanyabiashara kuona na kuchangamkia fursa mpya zilizopo ndani ya mkoa huo ili kujikwamua kiuchumi.

“Kuna fursa nyingi mkoani Geita ambazo zinahitaji watu waliopo tayari na waliopo rasmi kwenye mfumo wa biashara. Bila urasimishaji, ni vigumu kuzifikia fursa hizo,” amesema Luhumbi.

Faidha ambazo zinatokana na urasimishaji wa biashara ni kama vile Kupata uaminifu kutoka kwa wateja na washirika wa biashara, kuweza kufungua akaunti ya benki ya biashara, kustahili kupata mikopo au ufadhili kutoka taasisi za fedha, kulinda jina la biashara yako dhidi ya watu wengine kulitumia, kushiriki zabuni na fursa za biashara serikalini au taasisi binafsi na kufanya biashara kwa mujibu wa sheria na kuepuka usumbufu kutoka kwa mamlaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!