Latest Posts

WAKAZI WA SIRARI WATUMIA ALAMA YA CHANJO YA NDUI KUDHIBITI UANDIKISHAJI WA WAGENI

Wakazi wa mpaka wa Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara wamechukua hatua ya kutumia alama ya chanjo ya ndui kama njia ya kudhibiti uandikishaji wa wageni katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wakizingatia upekee wa alama hiyo kwa Watanzania.

Wananchi wa eneo hilo wamesema alama hiyo, ambayo ina tofauti kati ya Watanzania na Wakenya, inasaidia kwa urahisi kuwatambua wasio raia wa Tanzania. Wamebaini kuwa alama za chanjo kwa Watanzania zipo juu, wakati za Wakenya ziko chini, jambo linalorahisisha kutofautisha watu wa mataifa hayo mawili. Lugha pia imekuwa kigezo kingine muhimu katika utambuzi huo.

“Unajua ukiwaangalia wenzetu Wakenya, alama yao iko chini, sisi iko juu, kwa hiyo ni rahisi kuwagundua. Pia, lugha yao ya salamu ni tofauti na yetu, jambo ambalo limenisaidia kuandikisha Watanzania pekee,” alisema Mbasa Paul, mkazi wa Sirari.

Diwani wa Kata ya Sirari, Amos Sagara, alieleza kuwa wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa vijiji na wazee, pamoja na vyombo vya usalama, ili kuhakikisha watu sahihi pekee ndio wanaandikishwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, amesema zoezi hilo limehamasishwa kwa kasi na ana matumaini kwamba malengo waliyojiwekea yatafikiwa kwa ufanisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!